Duration 3:49

MAMBO MUHIMU UNAYOPASWA KUFANYA MARA BAADA YA KUKATALIWA AU KUACHWA KATIKA MAHUSIANO YA MAPENZI

17 175 watched
0
151
Published 5 Aug 2019

Unaweza kuwa ni miongoni mwa watu ambao wanateseka kutokana na mapenzi haijarishi ni kwa upande wa mwanamke au upande wa mwanaume siku zote maumivu huwa ni yaleyale, Watu wengi upitia wakati mgumu baada ya kutengana na yule ampendaye (mpenzi) Kuvunjika moyo na kukata tamaa ni moja ya mambo mazito na ambayo mtu hupitia na inahitaji sana kupiga moyo konde kwa sababu wakati huo mgumu ukiwa unaupitia. Fikra, mawazo mengi, maumivu na kujiona huna thamani ni baadhi ya vitu vinavyotokea pindi unapoakataliwa au kuachwa na mtu umpendaye lakini katika yote hayo yakupasa kufahamu ikiwa mtu kakukataa au kaamua kukuacha si lazima kumg’ang’ania cha msingi zingatia yafuatayo ambayo unapaswa kujifunza pale unapokuwa umeachwa; Ninayekuletea ndondoo hii ninaitwa Francesco Masangwa 1:Jifunze kuacha yapite. Muache aende kama alivotaka tambua duniani hayupo peke yake wapo wengi wamejaa kama yeye na unaweza kupata mzuri zaidi yake na ufurahie sana na kumshukuru Mungu. 2:Usikae peke yako kipindi hiki Jaribu kukaa na familia, marafiki na watu wako wa karibu, cheka na usiwe na uzuni furahia na chukulia ni jambo la kawaida hii ni moja ya safari ya kuanza kumsahau. 3:Usiwaze kwamba wewe ndio sababu Kama kuachana mmeshaachana, kwa nini ujilaumu? Mara nyingi mtu unayempenda akikuacha, kuna hali ya kibinadamu inakuja na unajikuta kama unatafuta mapungufu yako ili uweze kujilaumu. Hii haiwezi kukusaidia. hebu fikiria hata kama wewe ndio umesabababisha kukataliwa au kuachana kwenu, je ukishajilaumu ndio utakua umerudisha wakati nyuma ili mapenzi yenu yandelee kuwa moto moto? 4:Usifanye maamuzi yasiyo na mpango Mara nyingi watu hukasirika na kwenda kufanya sex hovyo hovyo pindi wanapotendwa au kuachwa na watu wanaowapenda. Tambua wazi hiyo sio njia sahii ya kutatua tatizo lako hebu fikiria hapo anayeumia ni nani? Utaenda kufanya sex na mtu mwingine kwa lengo la kulipiza kisasi kwa mtu ambaye hana mpango na wewe? Jitahidi sana kuepuka makundi ya watu ambao wanaweza kukuingiza kwenye mtego huu. Tafuta njia nyingine ya kutoa mawazo na kukupungizia stress. Jitahidi kufanya vitu il uwe na furaha na sio depression ukaja kufa bure siku sio zako ndugu. 5:Wekeza kwenye furaha yako Wataalamu wanasema mazoezi ni dawa ya vitu vingi sana mwilini. Jikite katika mazoezi mfano kukimbia au jiweke busy na kazi yoyote ili kukuweka busy na kupoteza mawazo kichwani kuhusu huyo mtu aliekuumiza, usijiumize kabisa. Ikiwa unajiona maumivu yanazidi, zidisha kujiweka busy na jiweke kama hujawahi kuumizwa na jipe moyo kuwa wewe kama wewe maana duniani hayuko peke yake. 6:Lenga kwenye mazuri yako Badala ya kuangalia mabaya ya kuvunjika uhusiano, wewe tizama yale mazuri tu uloyafanya, siku hizi unaweza kutendwa kweupee na huna kosa ulilolifanya, unajishangaa unakaushiwa tu,usijitie mnyororo wa roho buree ukasema hata nkitongoza naweza nisikae nae sana kama wa mwanzo. Wanaume wameumbiwa wanawake na wanawake wameumbiwa wanaume, hivyo basi hata ukiumizwa haifai kusema sitopenda tena au kusema sitokuja kutafuta mwenza tena, inamaana utaweza kukaa ivo pekeako mpaka uzeeni mpaka kufa. Tambua kuwa ni rahisi watu kuvutiwa na wewe endapo utakua unaonesha kama maisha unayamudu. Asante kwa kusikiliza hayo machache niliyokueleza na mambo haya yatakunufaisha zaidi ikiwa utayatumia. Ikiwa bado hujasubscribe katika chanel hii subscribe sasa ili uweze kupata mambo mengi zaidi #Faharimedia #FahariTv

Category

Show more

Comments - 8