Duration 4:40

RC KAFULILA AITAKA TAKUKURU SIMIYU KUZIFANYIA UCHUNGUZI AMCOS.

192 watched
0
2
Published 24 Jun 2021

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila ameitaka taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU Mkoani humo kufanya uchunguzi wa kina na kuzibaini Amcos zote ambazo zimeuza pamba kwa bei tofauti na ile aliyolipwa mkulima. Ametoa agizo hilo katika kikao kilichowakutanisha maafisa ushirika, wanunuzi wa pamba pamoja na serikali kwa ajili ya kujadili namna ya kumsaidia mkulima kulipwa pesa ya pamba kihalali pale anapouza mazao yake na kuondokana na ujanja ujanja unaofanywa na amcos hizo. Pia amewataka wakuu wa Wilaya kuchukua hatua kwa viongozi wote wa amcos watakaobainika kujihusisha na rushwa kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria na kwamba wanatakiwa kukamatwa. Awali wakizungumza katika kikao hicho baadhi ya wanunuzi wa pamba wamesema kuwa amcos zimekuwa zikifanya ujanja ujanja katika kuuza pamba ikiwemo kupokea rushwa jambo ambalo halimnufaishi mkulima na badala yake wanajinufaisha wao wenyewe. Emmanuel Mwelele ni mwenyekiti wa chama kikuu cha ushirika mkoani Simiyu (SIMCU), yeye amekiri kuwepo kwa tatizo la wakulima kulipwa fedha ambayo ni tofauti ya mauzo halisi ya pamba ambayo inauzwa kwa wanunuzi kutoka kwenye amcos kwa kile alichokieleza kuwa ni kutokana na tamaa.

Category

Show more

Comments - 0